Mji wa Newton hapa Marekani unaanza kazi ngumu ya mazishi ya watoto 20
na watu wazima 6 waliouwawa katika mashambulizi ya bunduki kwenye shule
ya msingi ya Sandy Hook huko katika jimbo la Connecticut.
Mazishi ya watoto wawili wa miaka 6 yatafanyika Jumatatu ya kwanza kwa
wale waliopigwa risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook katika mji
wa New town Connecticut. Watoto waliouwawa ijumaa walikuwa kati ya miaka
6 na 7.
Afisa wa Polisi alisema kwamba shule hiyo bado ni eneo la uhalifu na
wapelelezi bado wanafanya kazi saa 24 kwa ajili ya kesi hiyo. Amesema
watu wazima wawili walipigwa risasi lakini walinusurika kifo.
Rais Obama aliungana na waombolezaji huko New town Jumapili usiku ,
akiwaambia wale waliokusanyika kwenye ibada kuwa hawako peke yao kwenye
kuomboleza na taifa limeachwa na maswali magumu
Post a Comment