Van Gaal: ''FIFA imetuonea''
Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amelishutumu
shirikisho la soka duniani FIFA kwa "kufanya hila" kwa jinsi
linavyopanga ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia.
Wenyeji Brazil walicheza mechi mbili kabla ya
Uholanzi kucheza, lakini watacheza tena baada yake katika mechi ya
mwisho ya makundi, jambo ambalo Van Gaal anadai sio la haki.Sio jambo zuri," alisema Van Gaal ambaye huenda timu yake ikachuana na Brazil katika mechi za muondoano.
"Sio mchezo wa haki.''
''Nadhani katika Kombe la Dunia taifa linaloandaa mechi hizi hutendekezwa ."
watakaomaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi A walioko Brazil watachuana na watakaomaliza katika nafasi ya pili katika kundi B siku ya Jumamosi, huku atakayemaliza katika nafasi ya pili katika kundi A akimenyana na atakayemaliza katika nafasi ya B siku itakayofuata.
Post a Comment