“Mchungaji …yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’ wa ghafla wa mke wangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mke wangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako. Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!
Kwanza
ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mke wangu, lakini
kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni
tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe
rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!
Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mke wangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mke wangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hiyo accnt ipo nmb mwanza!
Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru
kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa
kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri
ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
Pia
napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa
taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa
na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao
wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na
aliyedeposit hizo fedha ni mmoja wa viongozi wako hapo kanisani!! Kuna
nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mke wangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi
nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika
mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mke wangu tulifikia hoteli
ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest
hill!!
Baada
ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwa
sababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu
waimbaji wote turejee dar es salaam!!
Lakini
uliniomba mke wangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu
maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na
nikamuacha mke wangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho
yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mke wangu arudi
hotelini kingsway!!
Kwaa
taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale
hotelini ni kuwa mke wangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa
chumba kililipiwa kwa siku zote zile!!
Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mke wangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote
haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini
nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa
yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii
sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!!
Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe
ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu
kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako
but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena,
nitakushinda.!!
Bila
kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta
ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya
ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki
je, uwahurumii hata watoto wetu??
Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama??
Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda

Yes
nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu
kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa
mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako
ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!!
Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu,
kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui
kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye
nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
Lakini
nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe
tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini
kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe
Hivi
kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili
wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata
mkewangu??
Naomba
uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi
mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku
mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini
kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya
tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua
kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana
tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani
tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu
upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka
hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki
wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa
dhambi hii!!
Kumbuka
kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari
pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta
loose!!
Mwisho
nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia
kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye
pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali
kwenye ukoo!!
Nakuonya
tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea
mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema
niachie mkewangu!!
Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya
watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya
kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha
kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe
ni nyoka!!
Sitakubali
kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!!
Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa
nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!
Nitapambana
na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu
wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti
na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia
yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana
kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..”
Post a Comment