Israeli imeendelea kuivirumishia makombora Gaza kucha
kutwa ,huku kikao cha mawaziri wa baraza la Usalama kikitarajiwa huko
Marekani kujadili mapendekezo mapya ya wito wa kusitishwa mapigano kwa
misingi ya kibinadamu.
Afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa
aliyeko Gaza Bob Turner, ameiambia BBC kuwa wapalestina laki moja unusu ,
ambao ni asilimia 8 ya idadi ya watu wa Gaza sasa wamekimbilia hifadhi
kwenye shule za Umoja wa mataifa.Idadi ya raia wa Palestina waliouawa imezidi mia nane, huku mashambulio hayo ya Israel ya angani majini na ardhini yakiingia siku ya kumi na nane.
Wanajeshi 32 na raia watatu wa Israel wameuawa katika muda huo.
Katika ukingo wa magharibi, na Jerusalem mashariki raia wawili wa Palestina wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati waandamanaji waliokuwa na hasira kuhusu mashambulio huko Gaza walipokabiliana na vikosi vya Israel.


Post a Comment