
Bwana Mahamat Kamoun alikuwa ameteuliwa na Bi Panza kwa niya ya kusitisha mapigano baina ya Wakristu na Waislamu ambayo yamepelekea kuuawa kwa maelfu ya watu katika taifa hilo katika kipindi cha mwaka mmoja uliyopita.
BwKamoun ni Waziri mkuu wa kwanza Muislamu katika bunge hilo linalotawaliwa na Wakristu waliowengi na anatarajiwa kuiongoza serikali ya mpwito.
Kulingana na Umoja wa Mataifa UN zaidi ya nusu ya watu nchini humo wanahitaji msaada wa hali na mali huku asilimia 20% wakiripotiwa kuwa wametoroka makwao kuepuka mapigano baina ya makundi ya Seleka na Anti-Balaka tangu mwaka wa 2013.
Mapigano yalianza pale Kiongozi wa waasi Seleka , Michel Djotodia, alipojiuzulu kama rais mwezi jJanuari mwaka huu kufuatia shinikizo la viongozi wa mataifa ya kanda ilikukomesha mapigano.
Lakini badala ya vita kupungua vilichacha zaidi makundi ya Wakristu walipoungana na kuanza kulipiza kiusasi dhidi ya jamii ya Waislamu waliowachache chini ya nembo ya Anti-Balaka.
katika kumkataa Kamoun Kundi la Seleka limesema kuwa aliwahi kuhudumu kaatika serikali ya Djotodia kama waziri wa Uchumi.
Alihudumu kama waziri wa fedha chini ya utawala wa aliyekuwa rais Francois Bozize ambaye aling'olewa mamlakani na waasi wa Kiislamu wa Seleka Machi 2013.

Chaguo la rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, la waziri mkuu lakataliwa na Seleka.
Baadaye akachaguliwa kama mshauri maalum wa Rais Catherine Samba Panza anayeongoza serikali ya mpito kwa sasa tangu Januari mwaka uliopita.
Wakristo , hasa wale wanaopinga Balaka wameridhika na uteuzi wake wakisema ni hatua ya kuleta maridhiano kati ya Wakristu na Waislamu nchini humo.
Hata hivyo, waliokuwa waasi wa Seleka , wanapinga wakisema ingekuwa vyema waziri mkuu kuwa mmoja wao.
Andre Nzapayeke, aliyekuwa waziri mkuu kabla ya uteuzi huu mpya, alijiuzulu hapo wiki jana siku ya Jumanne pamoja na mawaziri wake.
Rais Samba Panza, anasema uamuzi huo ulichukuliwa kulingana na makubaliano ya kusitisha mapigano yaliotiwa sahihi katika nchi ya Congo -Brazzavile mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Seleka yapinga waziri mkuu mteule.
Serikali mpya itatangazwa baada ya siku chache zijazo, lakini uwezekano wa kujumuishwa kwa vikundi vilivyojihami unaleta utata nchini humo.
Jukumu lake waziri mkuu itakuwa kuhakikisha kusitishwa kwa mapigano.
Vita kati ya wanaopinga kundi la Balaka na waliokuwa waasi wa Seleka vilisabisha vifo vya maelfu ya watu tangu mwaka uliopita.
Makundi hayo yalilaumiana kwa kutositishwa mapigano yalitokea kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo mwanzoni mwa wiki hii. Idadi kubwa ya waliokuwa waasi wa Seleka waliuawa kwenye vita hivyo vilivyohusisha jeshi la Ufaransa katika eneo la Batangafo.
Post a Comment